Sw

اَلنِّيَّةُ | Intentions

اَللَّهُمَّ إِنِّي نَوَيْتُ بِالصَّلَوٰةِ عَلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ امْتِثَالاً لِّأَمْرِكَ وَتَصْدِيقًا لِنَبِيِّكَ مُحَمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَمَحَبَّةً فِيهِ وَشَوْقًا إِلَيْهِ وَتَعْظِيمًا لِّقَدْرِهِ وَلِكَوْنِهِ أَهْلاً لِّذَلِكَ
Ee Allah, hakika nimekusudia kwa kumswalia Mtume (S.A.W) kuitikia amri Yako, kumsadikisha Mtume Wako Muhammad (S.A.W), kwa mapenzi na shauku kwake, na kuitukuza daraja yake na kwa kuwa yeye anastahiki hilo
فَتَقَبَّلْهَا مِنِّي بِفَضْلِكَ وَإِحْسَانِكَ وَأَزِلْ حِجَابَ الْغَفْلَةِ عَنْ قَلْبِي وَاجْعَلْنِي مِنْ عِبَادِكَ الصَّالِحِينَ.
Basi nikubalie kutoka kwangu kwa fadhila Zako na wema Wako, na uondoe pazia la mghafala katika moyo wangu, na unijaalie niwe miongoni mwa waja Wako wema
اَللَّهُمَّ زِدْهُ شَرَفًا عَلَىٰ شَرَفِهِ الَّذِيٓ أَوْلَيْتَهُ. وَعِزًّا عَلَىٰ عِزِّهِ الَّذِيٓ أَعْطَيْتَهُ.
Ee Allah, mzidishie utukufu juu ya utukufu wake uliomtunuku, na heshima juu ya heshima yake uliyompa
وَنُورًا عَلَىٰ نُورِهِ الَّذِي مِنْهُ خَلَقْتَهُ وَأَعْلِ مَقَامَهُ فِي مَقَامَاتِ الْمُرْسَلِينَ. وَدَرَجَتَهُ فِي دَرَجَاتِ النَّبِيئِينَ.
Na nuru juu ya nuru yake ambayo kwayo ulimuumba, na upandishe cheo chake katika vyeo vya Mitume, na daraja yake katika daraja za Manabii
وَأَسْئَلُكَ رِضَاكَ وَرِضَاهُ يَا رَبَّ الْعَالَمِينَ. مَعَ الْعَافِيَةِ الدَّآئِمَةِ وَالْمَوْتِ عَلَى الْكِتَابِ وَالسُّنَّةِ وَالْجَمَاعَةِ وَكَلِمَتَيِ الشَّهَادَةِ عَلَىٰ تَحْقِيقِهَا مِنْ غَيْرِ تَبْدِيلٍ وَّلَا تَغْيِيرٍ.
Na nakuomba radhi Zako na radhi zake, Ee Mola wa walimwengu, pamoja na afya ya kudumu na mauti katika Kitabu, Sunnah na Jamaa, na katika kuithibitisha shahada mbili pasina kubadilisha wala kugeuza
وَاغْفِرْ لِي مَا ارْتَكَبْتُهُ بِفَضْلِكَ وَجُودِكَ وَكَرَمِكَ يَآ أَكْرَمَ الْأَكْرَمِينَ.
Na unisamehe niliyoyatenda kwa fadhila Zako, upaji Wako, na ukarimu Wako, Ee Mbora wa wanaokirimu
وَصَلَّى اللَّهُ عَلَىٰ سَيِّدِنَا مُحَمَّدٍ خَاتَمِ النَّبِيِّينَ وَإِمَامِ الْمُرْسَلِينَ. وَعَلَىٰٓ ءَالِهِ وَصَحْبِهِ أَجْمَعِينَ. وَسَلَامٌ عَلَى الْمُرْسَلِينَ. وَالْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ.
Na rehema za Allah ziwe juu ya bwana wetu Muhammad, mwisho wa Manabii na imamu wa Mitume, na juu ya jamaa na maswahaba zake wote, na amani iwe juu ya Mitume, na sifa njema zote ni za Allah Mola wa walimwengu