عَلَى الْعَقِيقِ اجْتَمَعْنَا
Tulikutana kwenye Al-Aqiqi
Sw
عَلَى الْعَقِيقِ اجْتَمَعْنَا
نَحْنُ وَسُودُ الْعُيُونِ
Katika bonde la Aqiq tulikutana
Sisi na wenye macho meusi yenye haiba
مَا ظَنِّ مَجْنُونَ لَيْلَى
قَدْ جُنَّ بَعْضَ الْجُنُونِ
Ni nini dhana ya mpenzi wa Layla
Kwani amekumbwa na kiasi cha wazimu
فَيَا عُيُوني عَيَوْنِي
وَيَا جُفُونِي جَفَوْنِي
Enyi macho yangu mmenichosha
Na enyi kope zangu mmenitenga
وَيَا قُلَيْبِي تَصَبَّرْ
عَلَى الَّذِي فَارَقُونِي
Ewe kamoyo kangu fanya subira
Juu ya wale ambao wamenihama
فَارَقْتُهُمْ يَوْمَ الاِثْنَيْنِ
صُبْحَ الثَّلَاثَا وَاحِشُونِي
Niliagana nao siku ya Jumatatu
Jumanne asubuhi shauku ikanizidi
هُمْ سَادَةٌ خَلَّفُونِي
أَبْكِي دَماً مِنْ عُيُونِي
Wao ni watukufu walioniacha nyuma
Nikilia machozi ya damu
بَكَيْتُ حَتَّى رَثَانِي
الْطَّيْرُ فَوْقَ الْغُصُونِ
Nililia mpaka wakanisikitikia
Ndege walioko juu ya matawi
بِاللهِ إِنْ مُتُّ شَوْقاً
بِأَدْمُعِي غَسِّلُونِي
Kwa jina la Mungu nikifa kwa shauku
Kwa machozi yangu niosheni
نُوحُوا عَلَيَّ وَقُولُوا
هَذَا قَتِيلُ العُيُونِ
Nililieni na mkaseme
Huyu ni mhanga wa macho ya warembo
مَا زِلْتُ حَوْلَ الْمَطَايَا
أَقُولُ بِاللهِ احْمِلُونِي
Sikuchoka kuzizunguka ngamia
Nikisema: Kwa jina la Mungu nibebeni
إِلَى مَنَازِلِ قَوْمِي
سَارُوا وَمَا وَدَّعُونِي
Kuelekea maskani ya watu wangu
Walisafiri bila hata kuniaga
رُوحْ يَا رَسُولِي إِلَيْهِمْ
سِرْعاً وَقَبِّلْ يَدَيْهِمْ
Nenda ewe mjumbe wangu kwao
Kwa haraka na ukabusu mikono yao
وَاقْرَأْ سَلَامِي عَلَيْهِمْ
لَعَلَّهُمْ يَقْبَلُونِي
Na uwasomee salamu zangu
Ili huenda wakakubali kunipokea
جَانِي الْرَّسُول وَهُوَ يَضْحَكْ
وَقَالَ أَبْشِرْ بِصُلْحِكْ
Alinijia mjumbe huku akicheka
Akasema: Furahia kwa mapatano yako
وَحَيَاةِ عَيْشِكَ وَمِلْحِكْ
هُمْ بِالوِصَالِ وَاعَدُونِي
Kwa haki ya maisha yako na urafiki
Wameniahidi kukutana nami tena