بَحِبَّك وَ بَرِيْدَك
Nakupenda na Nakutamani
Sw
بَحِبَّك وَ بَرِيْدَك
وَاتْمَنَّى أَبُوس إِيدَك
Nakupenda na kukutamani
Na natamani kuibusu mikono yako
خَدَّامَك وَمُرِيدَك
يَا جَدَّ الْحَسَنَيْن
Mtumishi wako na mfuasi wako
Ee Babu wa al-Hasanayn
حَبِيْبِي مُحَمَّد
مَفِيشْ زَيُّه اتْنِين
Mpendwa wangu Muhammad
Hakuna aliye mfano wake
حُبُّه سَاكِن قَلْبِي
يَزِيد كُلِّ اتْنَيْنِ
Mapenzi yake yamekaa moyoni mwangu
Na yanazidi kila wakati
جَمَالُه وَ دَلَالُه
مِتْغَطِي بْجَلَالُه
Uzuri wake na madaha yake
Yamefunikwa na utukufu wake
وَتِقْعُد قْبَالُه
تُشُوفْهُم الِاتْنَيْن
Na ukiketi mbele yake
Unaviona vyote viwili pamoja
بَحِبَّك وَ بَرِيْدَك
وَاتْمَنَّى أَبُوس إِيدَك
Nakupenda na kukutamani
Na natamani kuibusu mikono yako
خَدَّامَك وَمُرِيدَك
يَا جَدَّ الْحَسَنَيْن
Mtumishi wako na mfuasi wako
Ee Babu wa al-Hasanayn
يَا أَجْمَل هَدِيَّة
مِنْ رَبِّ الْبَرِيَّة
Ee zawadi nzuri kabisa
Kutoka kwa Mola wa viumbe vyote
لِكُلِّ الدُّنْيَا دِيَّا
يَا جَدَّ الْحَسَنَيْن
Kwa ulimwengu huu wote
Ee Babu wa al-Hasanayn
مَاهْوِنْتَ قَمَرْهَا
وَانْتَ اللِّي مُنَوِرْهَا
Kwani wewe ni mwezi wake
Nawe ndiye unayeutia nuru
وَمْفَتَاح اسَرَارْهَا
يَا جَدَّ الْحَسَنَيْن
Na ufunguo wa siri zake
Ee Babu wa al-Hasanayn
بَحِبَّك وَ بَرِيْدَك
وَاتْمَنَّى أَبُوس إِيدَك
Nakupenda na kukutamani
Na natamani kuibusu mikono yako
خَدَّامَك وَمُرِيدَك
يَا جَدَّ الْحَسَنَيْن
Mtumishi wako na mfuasi wako
Ee Babu wa al-Hasanayn
حَبِيبِي وَعْنَيَّا
أَحْمَد ضَيّ عْنَيَّا
Mpendwa wangu na mboni yangu
Ahmad ni nuru ya macho yangu
أَنْتَ الْغَالِي عَلَيَّا
يَا جَدَّ الْحَسَنَيْن
Wewe ni mpendwa sana kwangu
Ee Babu wa al-Hasanayn
وَبِنْتَك الْبَتُول
يَا عُيُونَ الرَّسُول
Na binti yako, Al-Batul
Ee mboni ya macho ya Mtume
نَرْجُو مِنْكُم قَبُول
يَا جَدَّ الْحَسَنَيْن
Tunataraji kwenu kukubaliwa
Ee Babu wa al-Hasanayn
بَحِبَّك وَ بَرِيْدَك
وَاتْمَنَّى أَبُوس إِيدَك
Nakupenda na kukutamani
Na natamani kuibusu mikono yako
خَدَّامَك وَمُرِيدَك
يَا جَدَّ الْحَسَنَيْن
Mtumishi wako na mfuasi wako
Ee Babu wa al-Hasanayn
شُوفْتُه أَنِي قُصَادِي
اتْكَسَفْت أَنَادِي
Nilimwona akiwa mbele yangu
Nikaona haya kumwita
وِبْقَلْبِي سُهَادِي يَا جَدِّي
يَا جَدَّ الْحَسَنَيْن
Na moyoni nina mahangaiko, ee babu yangu
Ee Babu wa al-Hasanayn
يِنْدَهْلِي وَاجِيلُه
يِفْرِشْلِي مَنْدِيلُه
Ananiita nami namwendea
Ananikunjulia joho lake
حَبِيبِي أَنَادِيلُه
يَا جَدَّ الْحَسَنَيْن
Mpendwa wangu nanamwita
Ee Babu wa al-Hasanayn