صَفَتِ النَّظْرَهْ
Maono Yalikuwa Safi
Sw
صَفَتِ النَّظْرَهْ طَابَتِ الْحَضْرَةْ
جَاءَتِ الْبُشْرَى لِأَهْل اللهِ
Maono yametakata, hadhara imependeza
Imekuja bishara kwa ajili ya watu wa Allah
قَامُوْا سُكَارَى لِذِي الْبِشَارَه
جَعْلَوْا عِمَارَهْ شُكْراً لِلّهِ
Walisimama kama walevi kwa ajili ya bishara
Wakafanya dhikri ya kusimama kwa shukrani kwa Allah
أَيُّهَا الْحَاضِرْ اُذْكُرْ وَذَاكِرْ
إِيَّاكَ تُنْكِرْ حَالَ أَهْلِ اللهِ
Ewe uliyehudhuria, kumbuka na ukumbushe
Jihadhari usikanushe hali ya watu wa Allah
فَسَلِّمْ لَهُمْ فِيمَا عَرَاهُمْ
وَاعْلَمْ أَنَّهُمْ غَابُوْا فِي اللهِ
Basi jisalimishe kwao kwa yanayowakuta
Na ujue kwamba wao wametoweka ndani ya Allah
فَالْوَجْدُ بِهِمْ دَاعِيْ يَدْعِيْهِمْ
يَطْرَأْ عَلَيْهِمْ فِيْ ذِكْرِ اللهِ
Kwani wajadi ni mwitaji anayewaita
Huwajia ghafla katika dhikri ya Allah
وَمَنْ لَمْ يَجِدْ فَلْيَتَوَاجَدْ
قَصْداً يَتَعَرَّضْ لِفَضْلِ اللهِ
Na asiyepata wajadi, basi na auvute
Kwa makusudi akijielekeza kwenye fadhila za Allah
هَكَذَا قَالُوْا وَلِذَا مَالَوْا
وَلَقَدْ غَالُوْا فِي ذِكْرِ اللهِ
Hivyo ndivyo walivyosema na ndivyo wakayumba
Na hakika wamezama sana katika dhikri ya Allah
حَتَّى قَدْ ظَنَّا مَنْ لَيْسَ مِنَّا
أَنَّا جُنِنَّا بِذِكْرِاللهِ
Mpaka wakadhani wale wasio miongoni mwetu
Kwamba sisi tuna wazimu kwa dhikri ya Allah
هَنِيْئاً لَنَا ثُمَّ بُشْرَانَا
إِنْ كَانَ لَنَا حُمْقٌ فِي اللهِ
Hongera ni yetu na kisha bishara ni yetu
Ikiwa tuna uwendawazimu kwa ajili ya Allah