مَا لِلنِّيَاقِ إِذَا حَدَا جَمَّالُهَا
Kuna nini na ngamia pindi mchungaji wao anapowaimbia?
Sw
مَا لِلنِّيَاقِ إِذَا حَدَا جَمَّالُهَا
تَدَعُ الْعَنَاءَ وَلَا تَمَلُّ مَلَالَهَا
Wana nini hawa ngamia pindi mchungaji anapowaimbia?
Huuacha uchovu na wala hawachoshwi na safari
وَتَرَىٰ لَهَا فِي السَّيْرِ جِدًّا وَاضِحًا
شَوْقًا تَمُدُّ يَمِينَهَا وَشِمَالَهَا
Waona katika mwendo wao bidii iliyo dhahiri
kwa shauku wanajinyoosha kulia na kushoto kwao
وَتَبَاشَرَتْ لَمَّا أَتَتْ بَدْرًا رَأَتْ
نُورَ النَّبِيِّ الْهَاشِمِيِّ بَدَا لَهَا
Walishangilia walipofika Badr na kuona
nuru ya Nabii Mhashimi ikawadhihirikia
غَنِّ لَهَا يَا سَعْدُ بِاسْمِ مُحَمَّدٍ
فَلَعَلَّهَا تُصْغِي لِمَنْ غَنَّىٰ لَهَا
Waimbie, ee Sa'd, kwa jina la Muhammad
huenda wakamsikiliza yule anayewaimbia