مَا مَدَّ لِخَيْرِ الْخَلْقِ يَدَا
Extend Your Hand
Sw
الله الله الله الله الله الله
لَا إِلَٰهَ إِلَّا ٱللَّٰهْ
Allah Allah Allah Allah Allah Allah
Hapana mungu ila Allah
مَا مَدَّ لِخَيْرِ الْخَلْقِ يَدَا
أَحَدٌ إِلَّا وَبِهِ سَعِدَا
Hakuna aliyenyoosha mkono kwa mbora wa viumbe
ila tu kupitia kwake amepata kufuzu
فَلِذَاكَ مَدَدْتُ إِلَيْهِ يَدِي
وَبِذَلِكَ كُنْتُ مِنَ الْسُّعَدَا
Basi kwa ajili hiyo nimenyoosha kwake mkono wangu
na kwa hilo nikawa miongoni mwa wenye heri
بَابٌ لِلَّهِ سَمَا وَعَلَا
شَرَفاً وَامْتَازَ بِكُلِّ عُلَا
Ni mlango kuelekea kwa Allah uliotukuka na kupaa
kwa utukufu na ukapea katika kila kilele
وَالْكُلُّ بِدَعْوَتِهِ اتَّصَلَا
بِاللهِ وَحَازَ بِهِ الْمَدَدَا
Na wote kupitia mwito wake wameungana
na Allah na wakapata kupitia kwake msaada
إِنِّي فِي الْعُسْرِ وَفِي الْيُسْرِ
بِحِمَاهُ أَلُوذُ مَدَى الْعُمْرِ
Hakika mimi katika dhiki na katika faraja
katika himaya yake nakimbilia maisha yangu yote
وَأَقُولُ أَغِثْنِي يَا ذُخْرِي
وَأَنِلْنِي مِنْ كَفَّيْكَ نَدَا
Na nasema: "Ninusuru Ewe akiba yangu"
"na nistahilishe kutoka katika viganja vyako ukarimu"
وَعَلَيْنَا تَعَطَّفْ يَا أَمَلِي
بِشِفَاءِ الْقَلْبِ مِنَ الْعِلَلِ
Na tuonee huruma Ewe tumaini langu
kwa kuponya moyo kutokana na maradhi
أَيَكُونُ مُحِبُّكَ فِي وَجَلٍ
وَبِجَاهِكَ لَا أَخْشَى أَحَدَا
Je, mpenzi wako anaweza kuwa katika hofu?
Na kwa cheo chako simuogopi yeyote
لَا أَرْجُو غَيْرَكَ إِنْ جَارَا
دَهْرِي وَعَدِمْتُ الْأَنْصَارَا
Simtarajii yeyote ghairi yako zama zikinisonga
na ninapokosa kabisa wa kuninusuru
بِحَيَاتِكَ أَلْقِ الأَنْظَارَا
كَرَماً يَا أَفْضَلَ مَنْ سَجَدَا
Kwa uhai wako tupa jicho la huruma
kwa ukarimu Ewe mbora wa waliosujudu
أَنْتَ الْمُخْتَارُ مِنَ القِدَمِ
يَا خَيْرَ شَفِيعٍ فِي الأُمَمِ
Wewe ndiwe mteule tangu asili
Ewe mwombezi mbora miongoni mwa umma
وَبِنُورِكَ مِنْ بَعْدِ الْعَدَمِ
وَجْهُ الْتَّكْوِينِ زَهَا وَبَدَا
Na kwa nuru yako baada ya kutokuwepo
uso wa uumbaji uling'ara na kudhihiri
وَصَلَاةُ اللهِ بِلَا حَصْرِ
لَكَ تُهْدَى يَا سَامِي الْقَدْرِ
Na rehema za Allah zisizo na idadi
kwako zinaletwa zawadi Ewe mwenye daraja ya juu
وَالْآلِ مَعَ الْصَّحْبِ الْغُرِّ
مَا حَادِي الْعِيسِ نَشَا وَصَدَى
Na kwa jamaa zako na maswahaba waungwana
madhali mwongoza-ngamia anaimba na kuitika