لِي فِي المَدِينَةِ أَحْبَابٌ إِذَا نَظَرُوا
I Have Beloveds In Medina; When They Gaze Upon Me
Sw
لِي فِي المَدِينَةِ أَحْبَابٌ إِذَا نَظَرُوا
إِلَيَّ وَلَّتْ هُمُومِي وَانْجَلَى الضَّرَرُ
Nina wapendwa Madina ambao wakinitazama
Ghamu zangu hutoweka na dhiki huniondoka
وَأَصْبَحَ القَلْبُ فِي أُنْسٍ وَفِي فَرَحٍ
جَمٍّ وَصَاحَبَنِي التَّوْفِيقُ وَالظَّفَرُ
Na moyo huwa katika utulivu na furaha
tele, nami hufuatana na taufiki na ushindi
يَا أَهْلَ طَيْبَةَ هَيَّا إِنَّنِي دَنِفٌ
وَإِنَّنِي لِلَّذِي أَمَّلْتُ مُنْتَظِرُ
Enyi watu wa Taiba fanyeni haraka kwani mimi ni mgonjwa
na kile nilichokitarajia mimi nakisubiri
جَرَتْ عَوَائِدُكُمْ أَنَّ المُحِبَّ إِذَا
نَادَاكُمُ بِلِسَانِ الحُبِّ يَنْجَبِرُ
Ni desturi yenu kwamba mwenye kupenda pindi
akiwaita kwa ulimi wa mahaba hufarijika
وَالحُبُّ مِلْءُ جَنَانِي بَلْ تَجَسَّمَ فِي
شَخْصٍ عَلَى صُورَتِي إِنْ دَلَّتِ الصُّوَرُ
Mahaba yamejaa kifuani mwangu bali yameumbika
katika nafsi ya sura yangu pindi sura zikidhihiri
يَا سَيِّدَ الرُّسْلِ أَدْرِكْنِي فَمَا بَقِيَتْ
لِي حِيلةٌ غَيْرُ حُبٍّ مِنْكَ مُدَّخَرُ
Ewe bwana wa Mitume nidiriki kwani hakukubaki
kwangu mbinu ila pendo lako nililoweka akiba
لِلَّهِ مِيلادُكَ الغَالِي الذِي سَعِدَتْ
بِهِ البَسِيطَةُ وَانْجَابَتْ بِهِ الغِيَرُ
Kwa ajili ya Mungu ni mazazi yako adhimu ambayo
ardhi ilifurahi kwayo na mazito yakaondoka
يَوْمٌ بِهِ ضَاءَتِ الدُّنْيَا فَمَا طَلَعَتْ
شَمْسٌ عَلَى مِثْلِهِ فِيهَا وَلَا قَمَرُ
Siku ambayo kwayo dunia iliangaza na halijachomoza
jua mfano wake kamwe wala mwezi
تَحِيَّةٌ لَكَ مِنْ قَلْبٍ مُعَطَّرَةٌ
يَزِيدُ عَرْفَ شَذَاهَا رَوْحُكَ العَطِرُ
Salamu kwako toka moyoni zenye manukato
harufu yake huzidishwa na roho yako yenye harufu nzuri
وَقَائِلٍ لِيْ مَا تَشْتَاقُ قُلْتُ لَهُ
أَشْتَاقُ طَيْبَةَ شَوْقاً لَيْسَ يَنْحَصِرُ
Na anayeniuliza "Unatamani nini?" nikamwambia
naitamani Taiba kwa shauku isiyo na mwisho
يَا قَائِدَ الجَوِّ أَنْزِلْنِي إِذَا لَمَعَتْ
لِعَيْنِكَ القُبَّةُ الخَضْرَاءُ وَالحُجَرُ
Ewe rubani wa angani nishushe pindi itakapoangaza
machoni pako ile Kuba ya Kijani na vyumba vile
هُنَاكَ أَقْصِدُ شُبَّاكَ الرَّسُولِ لِكَي
أَسْتَغْفِرُ اللهَ حَيْثُ الذَّنْبُ يُغْتَفَرُ
Hapo nitaelekea kwenye dirisha la Mtume ili
nimuombe Mungu msamaha ambapo dhambi husamehewa
عَلَيْكَ صَلَاةُ اللهِ مَا تُلِيَتْ
فِي حَفْلِ مِيلادِكَ الآياتُ والسُوَرُ
Rehema za Mungu ziwe juu yako kila yanaposomwa
katika hafla ya mazazi yako aya na sura
والآلِ والصَحْبِ وَالأَتْبَاعِ قَاطِبَةً
والغَوثِ والقطبِ والأحبَابِ إذْ حَضَرُوا
Na jamaa na maswahaba na wafuasi wote
na Ghawthi na Qutbi na wapendwa waliohudhuria