نَسِيْمْ هَبَّتْ عَلَيْنَا مِنْ حِمَى الْمُصْطَفَى
Upepo Mwanana Uliotuvumia Kutoka Himaya ya Al-Mustafa
Sw
Sw
نَسِيْمْ هَبَّتْ عَلَيْنَا مِنْ حِمَى الْمُصْطَفَى
نَسِيْمْ فِيْهَا الْهَنَا فِيْهَا الْدَّوَا وَالْشِّفَا
Upepo mwanana umetuvumia kutoka maskani ya Mteule
Upepo wenye neema, dawa, na ponyo
بِشَمِّهَا يَصْلُحُ الْظَّاهِرْ لَنَا وَالْخَفَا
يَا بَخْتَ مَنْ لِلْنَّبِي فِي كُلِّ حَالٍ اقْتَفَى
Kwa kunusa harufu yake, dhahiri na siri zetu hutengenea
Ah, heri kwa yule anayemfuata Mtume katika kila hali!
عَلَى قَدَمْ صِدْقْ مَعَ أَهْلِ الْهِمَمِ وَالْوَفَا
هُمُ الْرِّجَالُ الْأَكَابِرْ هُمُو هُمُو الْشُّرَفَا
Kwa mguu wa ukweli pamoja na watu wenye azma na uaminifu
Wao ndio watu wakuu, hakika wao ndio watukufu
هُمْ أَهْلُ الْأَسْرَارِ هُمْ أَهْلُ الْنَّقَا وَالْصَّفَا
يَا حَادِيَ اسْجَعْ فَحَالِي بِالنَّبِي قَدْ صَفَا
Wao ni watu wa siri, watu wa utakaso na usafi
Ewe mwongoza ngamia, imba! Kwani hali yangu kwa Mtume imekuwa safi
إِذَا بَدَتْ عَيْنُ جُوْدِ اللهِ عَنَّا عَفَى
اللهُ حَسْبِي وَنِعْمَ الْحَسْبُ حَسْبِي كَفَى
Chemchemi ya ukarimu wa Allah ikidhihiri, hutusamehe
Allah ananitosha; na ni Mtoshelezi mbora kabisa!
مِنْهُ الْمَوَاهِبْ وَمِنْهُ الْعَافِيَهْ وَالشِّفَا
يَا وَاسِعَ الْجُوْدِ رَبِّي خَيْرُ عَافِي عَفَى
Kwake hutoka mapaji, na kwake hutoka afya na ponyo
Ewe Mwingi wa ukarimu, Mola wangu ni mbora wa wanaosamehe
امْنُنْ عَلَيْنَا بِرُفْقَةِ عَبْدِكَ الْمُصْطَفَى
اسْلُكْ بِنَا نَهْجَ مَنْ لِهَدْيِهِ اقْتَفَى
Tufadhili kwa usuhuba wa mja Wako Mteule
Na utuongoze katika njia ya wale waliofuata uongofu wake
نَثْبُتْ فِيْهِ وَلِوِرِّاثِ الْنَّبِي الْخُلَفَا
بِجَاهِ أَحْمَدَ حَبِيْبِ اللهِ كَنْزِ الْوَفَا
Ili tudumu kwayo, na kuwafuata warithi na makhalifa wa Mtume
Kwa utukufu wa Ahmad, mpenzi wa Allah, hazina ya uaminifu
عَلَيْهِ صَلَّى إِلَهِي مَا الْحَيَا وَكَفَى
وَالْآلِ وَالْصَّحْبِ مَا بَرْقُ الْسَّمَا رَفْرَفَا
Rehema za Mola ziwe juu yake madamu mvua inanyesha na kutosha
Na jamaa na maswahaba, madamu umeme unamulika mbinguni