يَا وَاهِبَ الْإِنْسَانِ أَسْبَابَ الْهُدَى
Ee Mpaji wa Mwanadamu Sababu za Uongofu
Sw
يَا وَاهِبَ الْإِنْسَانِ أَسْبَابَ الْهُدَى
يَا مَنْ بِحَمْدِ الْعَالَمِينَ تَفَرَّدَا
Ewe Mtoaji wa nyenzo za uongofu kwa mwanadamu
Ewe Ambaye pekee Unastahili sifa za walimwengu
لِي عِنْدَ بَابِكَ يَا إِلَهِي دَعْوَةٌ
فِيهَا رَجَاءُ الْعُمْرِ جَاءَ مُجَسَّدَا
Nina ombi mlangoni Pako, Ee Mungu wangu
Ambamo tumaini la maisha yangu limechukua sura
أَنْتَ الَّذِي مَا خَابَ عِنْدَكَ سَائِلٌ
أَيَكُونُ بَابُكَ دُونَ سُؤْلِي مُؤْصَدَا
Wewe ndiye Ambaye mwombaji hakati tamaa Kwako
Je, yawezekana mlango Wako ukafungwa mbele ya haja yangu?
فَبِفَضْلِكَ اللَّهُمَّ عِشْتُ مُوَحِّدا
أَيُرَدُّ عِنْدَكَ مَنْ أَتَاكَ مُوَحِّدَا
Kwa fadhila Zako Ee Allah nimeishi nikikiri Upweke Wako
Je, atafukuzwa Kwako yule anayekujia hali ya kukupwekesha?
سُؤْلِي كَذَاتِكَ وَاحِدٌ فَبِحَقِّهَا
لَوْ لَحْظَةً دَعْنِي أُشَاهِدَ أَحْمَدَا
Hitaji langu ni moja kama ilivyo Dhati Yako, basi kwa haki ya Upweke huo
Niruhusu, japo kwa kitambo, nimtazame Ahmad