هَذَا الْمَقَامُ الَّذِي لَاذَتْ بِهِ الْأُمَمُ
Hiki ndicho cheo ambacho mataifa yamekikimbilia.
Sw
هَذَا الْمَقَامُ الَّذِي لَاذَتْ بِهِ الْأُمَمُ
وَأَذْعَنَتْ لِعُلَاهُ الْعُرْبُ وَالْعَجَمُ
Hiki ndicho cheo ambacho mataifa yamekitafuta hifadhi
Na Waarabu na wasio Waarabu wakanyenyekea utukufu wake
هَذَا مَقَامُ رَسُولِ اللَّهْ أَكْرَمُ مَنْ
جَاءَتْهُ مِنْ رَبِّهِ الْأَحْكَامُ وَالْحِكَمُ
Hiki ni cheo cha Mjumbe wa Allah, mbora wa wale
Ambao hukumu na hekima zimemjia kutoka kwa Mola wake
هَذَا مُحَمَّدُ الْهَادِي الَّذِي مُحِيَتْ
عَنَّا بِنُورِ هُدَاهُ الْظُّلْمُ وَ الْظُّلَمُ
Huyu ndiye Muhammad Mwongozi ambaye yamefutwa
Kwetu kwa nuru ya uongofu wake dhuluma na kiza
هَذَا الَّذِي قَدْ سَمَا فَوْقَ الْسَّمَا
إِلَى مَقَامِ عِزٍّ تَنَاهَتْ دُونَهُ الْأُمَمُ
Huyu ndiye aliyepanda juu zaidi ya mbingu
Kwenye daraja ya enzi ambayo mataifa yameshindwa kuifikia
يَا سَيِّدِي يَا رَسُولَ اللَّهْ يَا أَمَلِي
يَا مَنْ أَلُوذُ بِهِ إِنْ زَلَّتِ الْقَدَمُ
Ewe bwana wangu, ewe Mjumbe wa Allah, ewe tumaini langu
Ewe ambaye kwake nakimbilia pindi mguu utakapoteleza
بِكَ اهْتَدَيْتُ إِلَى الْإِيمَانِ فَاتَّصَلَتْ
بِذَاكَ عِنْدِي مِنْ أَفْضَالِكَ الْنِّعَمُ
Kwako nimepata uongofu wa imani, kisha zikaandamana
Kwangu neema kutokana na fadhila zako
صَلَّى عَلَيْكَ إِلَهُ الْخَلْقِ مَا سَجَعَتْ
وَرْقٌ وَمَا هَطَلَتْ مِنْ سُحْبِهَا دِيَمُ
Rehema za Mungu wa viumbe ziwe juu yako muda njiwa wanapoimba
Na muda mvua za kudumu zinapomiminika kutoka mawinguni