مَعَانِي قَدْ بَدَتْ عِنْدِي غَرِيبَهْ
Maana za ajabu zimenipambazukia
Sw
مَعَانِي قَدْ بَدَتْ عِنْدِي غَرِيبَهْ
وَمَا تُفْضِي إِلِيْهْ بَعْدُ أَغْرَبْ
Maana zimenibainikia zikiwa ngeni na adhimu
Na mwisho uelekeao ni wa ajabu zaidi
مِنَحْ مِنْ فَضْلِ مَوْلَانَا عَجِيبَهْ
وَمَاذَا فِي عَطَاهُ لَيْسَ أَعْجَبْ
Ni tunu za fadhila za Mola wetu za kustaajabisha
Na kipi katika kutoa Kwake kisichokuwa cha ajabu?
وَعِيدُ الْصَّبِ أَنْ يَلْقَى حَبِيبَهْ
وَسُبْحَانَ الَّذِي قَرَّبْ وَحَبَّبْ
Furaha ya mpenzi ni kukutana na Mpendwa wake
Na atakasike Yule aliyetukurubisha na kutupa mahaba
مَعِي أَقْوَامْ فِي أَعْلَى كَتِيبَهْ
لَهُمْ أَسْرَارْ لَا تُحْصَى وَتُكْتَبْ
Pamoja nami ni watu katika kundi la daraja za juu
Wana siri zisizoweza kudhibitiwa wala kuandikwa
مَوَاهِبْ عَالِيَةْ مَا هِيْ كَسِيبَهْ
وَإِحْسَانُ الْمُهَيْمِنْ لَيْسَ يُحْسَبْ
Ni vipaji vya juu, si vya kuchuma kwa juhudi
Na wema wa Mlinzi Mwenye Enzi hauwezi kukadirika
وَمَنْ لُهْ سَابِقَهْ يُدْرِكْ نَصِيبَهْ
مُوَفَّى دُونَ أَنْ يَشْقَى وَيَتْعَبْ
Na mwenye kudra iliyotangulia atapata fungu lake
Akizawidiwa kikamilifu bila kutaabika wala kuchoka
وَنَفْحَةُ بَاسِطِ الْنَّعْمَى قَرِيبَهْ
تَعَرَّضْ يَا فَتَى مِنْهَا تَقَرَّبْ
Na upepo mwanana wa Mwenye Kukunjua neema uko karibu
Jilekeze kwayo ewe kijana na upate kukurubia
عَسَى الْمَكْلُومْ أَنْ يَلْقَى طَبِيبَهْ
فَيُضْحِي الْعِيْشْ لُهْ أَطْيَبْ وَأَطْيَبْ
Huenda aliyejeruhiwa akakutana na tabibu wake
Maisha yakawa kwake matamu na mazuri zaidi
وَصَلَّى اللهُ مَا أَفْهَامٌ نَجِيبَهْ
وَعَتْ قَوْلاً بِمَاءِ الْعَيْنِ يُكْتَبْ
Rehema za Allah ziweko maadamu akili tukufu
Zimefahamu maneno yanayostahili kuandikwa kwa machozi
عَلَى خَيْرِ الْوَرَى الْهَادِي حَبِيبِهْ
وَآلِهْ وَالَّذِي لِلْطُّهْرِ يَصْحَبْ
Kwa mbora wa viumbe, Mwongozaji, Mpendwa Wake
Na jamaa zake na kila aliyefuatana naye kwa usafi