ْيَاجَمَالُه
Oh, How Beautiful He Is!
Sw
آه يَا جَمَالُه يَا جَمَالُهْ
سِيدْنَا النَّبِى يَا جَمَالُهْ
Ah, uzuri wake! Ah, uzuri wake!
Ah, uzuri wake! Ah, uzuri wake!
سِيدْنَا النَّبِى يَا جَمَالُهْ
Bwana wetu Mtume, ah uzuri wake!
كَحِيلُ الطَّرْفِ حَبِيبِي لَوْ تَرَاهُ
ضَحُوكُ السِّنِّ لِلْعَاشِقِ رَمَاهُ
Mpenzi wangu ana macho ya wanja, laiti ungemuona!
Mwenye tabasamu angavu, humtumbukiza mpenzi katika mshangao wa mahaba
بَهِيُّ الطَّلْعَةْ فَالْمَوْلَى اصْطَفَاهُ
وَكُلُّ الْخَلْقِ أَنَارَ بِنُورِ طه
Mwenye sura yenye nuru, Mola amemteua
Na viumbe vyote vimeangazwa kwa nuru ya Taha
وَلَا ظِلُّ لَهُ بَلْ كَانَ نُوْرَا
تَنَالَ الشَّمْسُ مِنْهُ هُوَ الْبُدُوْرَ
Hakuwa na kivuli, bali alikuwa nuru
Jua huchota mwangaza kwake, naye ni mwezi mpevu
وَلَمْ يَكُنِ الْهُدَى لَوْلَاهُ ظُهُوْرَا
وَ كُلُّ الْكَوْنِ أَنَارَ بِنُوْرِ طَــــــهَ
Isingekuwa yeye, uongofu usingedhihirika
Na ulimwengu mzima umeangazwa kwa nuru ya Taha
وَكَفُّ الْمُصْطَفَى كَالْوَرْدِ نَادِى
وَعِطْرُهَا يَبْقَى إِذَا مَسَّتْ أَيَادِى
Kiganja cha Mteule ni kama waridi bichi lenye umande
Na harufu yake hubaki mikononi inayokigusa
وَعَمَّ نَوَالُهَا كُلَّ الْعِبَادِ
حَبِيبُ اللهِ يَا خَيْرَ الْبَرَايَا
Karama zake zimewafikia waja wote
Ewe mpenzi wa Allah, ewe mbora wa viumbe vyote!
وَرِيقُ الْمُصْطَفَى يَشْفِي الْعَلِيلَ
وَعَيْنُ قَتَادَةَ خُذْهَا دَلِيلًا
Mate ya Mteule huponya wagonjwa
Chukua jicho la Qatadah kama ushahidi wa hili
تَفَلَ فِي الْبِئْرِ أَضْحَتْ سَلْسَبِيلًا
وَصَارَ لِصَحْبِهِ شَهْدًا مُدَامًا
Alitemea mate kisimani kikawa chemchemi
Na kwa masahaba zake ikawa tamu kama asali inayodumu