لِغَيْرِ جَمَالِكُمْ نَظَرِي حَرَامُ
Kwa asiyekuwa uzuri wenu, mtazamo wangu ni haramu.
Sw
لِغَيْرِ جَمَالِكُمْ نَظَرِي حَرَامُ
وَغَيْرُ كَلَامُكُمْ عِنْدِي كِلَامُ
Kutazama uzuri usio wenu kwangu ni haramu
na yasiyokuwa maneno yenu kwangu si maneno
وَعُمْرُ الْنَّسْرِ مِنْكُمْ بَعْضُ يَوْمٍ
وَسَاعَةُ غَيْرِكُمْ عَامٌ فَعَامُ
Umri wa tai pamoja nanyi ni sehemu ya siku
na saa moja kwa wengine ni miaka na miaka
وَصَبْرِي عَنْكُمُ شَيْءٌ مُحَالٌ
وَمَا لِي قَاتِلٌ إِلَّا الْفِطَامُ
Na subira yangu mbali nanyi ni jambo muhali
na sina muuaji mwingine ila ni kutengwa nanyi
إِذَا عَايَنْتُكُمْ زَالَتْ هُمُومِيْ
وَإِنْ غِبْتُمْ دَنَا مِنِّيْ الْحِمَامُ
Pindi nikiwaoneni huzuni zangu hutoweka
na mkiondoka mbali nami mauti hunikaribia
أَوَدُّ بِأَنْ أَكُونَ لَكُمْ جَلِيسًا
وَتُنْصَبَ لِي بِرَبْعِكُمُ خِيَامُ
Natamani niwe mwenye kuketi pamoja nanyi
na hema zangu zipigwe katika makazi yenu
فَدَاوُوا بِالْوِصَالِ مَرِيضَ هَجْرٍ
يَهِيمُ بِكُمْ إِذَا سَجَعَ الْحَمَامُ
Basi ponyeni kwa kuungana nanyi mgonjwa wa kutengwa
anayeweweseka nanyi njiwa wanapoimba kwa mahadhi
حَدِيثُ غَرَامِهِ فِيكُمْ قَدِيمٌ
وَمَلْبَسُهُ مِنَ الْحُبِّ الْسِّقَامُ
Habari ya mapenzi yake kwenu ni ya tangu kale
na vazi lake kutokana na pendo ni maradhi
فَأَنْتُمْ فِي الْأُصُولِ أَجَلُّ أَصْلٍ
إِذَا شِئْتُمْ تَحَصَّلَ لِي الْمَرَامُ
Kwani ninyi katika asili ni asili tukufu kabisa
mkitaka ninyi, basi nitayapata matamanio yangu
بِكُمْ صَعْبُ الْأُمُورِ يَعُودُ سَهْلًا
فَبِالْإِحْسَانِ جُودُوا يَا كِرَامُ
Kwenu ninyi mambo magumu hugeuka kuwa mepesi
basi fanyeni ukarimu kwa ihsani enyi watukufu
وَلَيْسَ سِوَاكُمُ لِلْجُودِ أَهْلًا
فَكَيْفَ نَزِيلُ سُوحِكُمُ يُضَامُ
Na hakuna mwingine ila ninyi anayestahili ukarimu
basi vipi mgeni wa uwanja wenu adhulumiwe?